CCM, Chadema waanza kujinadi uchaguzi mitaa K’njaro

KATIBU wa NEC, Siasa na Uhusi ano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid

KATIBU wa NEC, Siasa na Uhusi ano wa Kimataifa (SUKI) na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Rabia Hamid amewataka wakazi wa Kilimanjaro kuwachagua wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho juzi katika viwanja vya Pasua, Rabia alisema CCM imeendelea kuwahudumia wananchi katika sekta zote, hivyo wananchi hawana budi kuwachagua viongozi wali otokana na chama hicho.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho amemtuma kuwataka wanan chi wawachague wagombea wa chama hicho ili wawaletee maendeleo.

Advertisement

“Mambo mengi ya maendeleo yamefanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro ambayo wananchi wenyewe wanashuhudia ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya, shule pamoja na miundombinu ya barabara na yote ni kutokana na uimara wa CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo,” alisema.

Soma pia: Uchaguzi mitaa kutumia 4R za Rais za Samia

Awali, Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Patrick Bois afi aliwapongeza wananchi wote waliojiandikisha na kushiriki katika kura za maoni na sasa wanakwenda kutafuta ushindi.

Wakati huohuo, Chama cha Demokrasia na Maende leo (Chadema) Moshi mkoani hapa kimezindua kampeni hizo kwa kuja na mpango wa Operesheni ‘OMO’ ili kujinyakulia nafasi za uongozi serikali za mitaa.

Akizungumza na wanan chi waliojitokeza kusikiliza sera na kuwatambua viongozi wanaowania nafasi za uongozi katika eneo la Njoro ya reli Manispaa ya Moshi, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basili Lema ali yeongoza ufunguzi wa kam peni hizo, aliwataka wananchi kujitokeza kupiga kura na kuunga mkono opereshi hiyo ili kupata viongozi waadilifu.