CCM kuimarisha sekta ya madini Singida

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kwamba katika kipindi cha miaka mitano ijayo, endapo kitapewa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi, kitaimarisha zaidi sekta ya madini mkoani Singida kwa kuanzisha masoko mapya ya madini katika maeneo ya Sekenke na Puma na kuendeleza soko la Shelui.

Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Ilongero mkoani Singida juzi jioni, ambapo alibainisha kwamba chama hicho kimeweka mpango mahsusi wa kuongeza fursa za uchimbaji, biashara na uongezaji thamani wa madini nchini.

Alisema kwa sasa tafiti za madini zinazotekelezwa nchini zinahusisha takribani asilimia 16 pekee ya maeneo yote, lakini katika awamu ijayo CCM imelenga kuongeza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 50 ili kutoa nafasi kwa vijana wengi kushiriki katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini.

“Katika ilani yetu tumesema wazi tutahakikisha sekta ya madini inapanuka zaidi, vijana wetu wapate ajira, wawe na fursa za kutosha katika biashara na uongezaji thamani wa madini. Tutaimarisha masoko yaliyopo kama Shelui na kuanzisha masoko mapya Sekenke na Puma ili kuinua uchumi wa wananchi,” alisema Dk Nchimbi

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button