CCM wafunga kampeni kwa kishindo Bukoba

BUKOBA: Maelfu ya wananchi na wadau wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Bukoba Mjini wameshuhudia kampeni za mgombea ubunge CCM, Mhandisi Johanseni Mtasingwa zimehitimishwa kwa kishindo ikiwa ni siku moja kabla ya kupiga kura.

Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Mjini Mhandisi Mtasingwa amewahakikishia wanachi kuwa atashirikiana na serikali kukamilisha miradi yote ilianzishwa na kuanzisha mipya.

“Najua Kuna stendi kuu soko la Bukoba ,kingo za mto kanoni miundombinu ya Barabara na kupendezesha mji wa Bukoba nitazitekeleza ,nitatekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi na kuwa mtumishi wenu
Viongozi mbalimbali wa CCM wamenadi Ilani na sera za chama hicho ambapo wamewaomba wanachi kuchagua chama Cha Mapinduzi kwa Ngazi za ubunge Uraisi na udiwani.



