CCM yarekebisha Katiba, yaongeza wajumbe majimboni

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya marekebisho ya mbalimbali ya Katiba ya CCM ya 1977 ikiwamo ya kuongeza idadi ya wajumbe wanaopiga kura za kuteuwa wagombea wa udiwani, ubunge na uwakilishi.

Akifafanua mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan alisema marekebisho hayo yanaongeza idadi ya wajumbe wanaingia katika Halmashauri Kuu wa CCM Taifa ili kuongeza sauti za wananchi kwa kuongeza idadi ya wanaCCM huku wajumbe wengine wakiingia kwa nafasi zao.

Alisema marekebisho mengine ni utaratibu wa kupigakura na kuwa mabadiliko hayo ni kushughulika na wajumbe wanaofanya kazi ya kuteuwa wagombea.

“Imebidi kuongeza idadi ya wapigakura ili kutanua demokrasi kwa wanaCCM, kuweka uwanja mpana wa kuchangua wawakilishi wa eneo, tukiongeza idadi hii inaaminika kwamba sauti ya wanaCCM katika eneo lile itakuwa imekuwa na wamemchangua mtu ambaye anakubarika na wengi, ndio kiini cha mapendekezo hayo.

“Watakuwa ni wajumbe wengi kidogo, wale wanaopenda kucheza na wajumbe wajipange,” alisema. Pia, mabadiliko hayo yanakwenda katika utaratibu wa kuchuja wagombea itapandisha ngazi ya juu wagombea watatu labda kamati itaona vinginevyo.

Akiwasilisha mapendekezo kwenye mkutano huo, Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni, Issa Gavu alisema lengo la mabadiliko hayo ni kuongeza ushiriki wa wanachama kufanya maamuzi, kuimarisha muundo wa ngazi ya shina pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa.

Marekebisho hayo yaliyopitishwa jana katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa jijini Dodoma ambayo yameongeza idadi ya wajumbe wa kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka sita na kuwa wajumbe 10.

Pia, kuongeza idadi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa kata/wadi, jimbo na wilaya kwa ajili ya kupiga kura za maoni kuwapendekeza wanachama wanaogombea nafasi ya udiwani, ubunge au uwakilishi wa eneo husika. Na pia utaratibu wa kuchuja wagombea, watachujwa na vikao ambavyo vitateua majina yasiyozidi matatu na yatarudishwa kupigiwa kura za maoni.

Alisema Ibara zilizoguswa na marekebisho hayo ni Ibara ya 9 imeondoa sharti la mtu anayetaka kuwa mwanachama kujaza fomu na sasa atawasilisha maombi kwa Katibu wa Tawi mahali anapoishi.

Pia, Ibara ya 22 (2) (a) na (b), utambuzi wa mashina umebadilishwa kwa Tanzania Bara sasa litaundwa na wanachama wanaotoka kwenye nyumba zilizopo kwenye eneo moja zisizopungua 10 na zisizozidi 20 zenye wanachama wasiopungua 50 na wasiozidi 80 kwa maeneo ya mijini na wasiopungua 30 na wasiozidi 80 kwa maeneo ya vijijini.

Alisema kwa upande wa Zanzibar, Shina litaundwa na wananchama wanaotoka kwenye nyumba zilizopo kwenye eneo moja zisizopungua 10 na zisizo zidi 20 zenye wananchama wasiopungua 20 na wasizozidi 30 Pia, wameongeza kifungu cha 47 (1) (s) kwa madhumuni ya kupiga kura za maoni kwa lengo la kuwezesha wajumbe wote wa kamati ya siasa ya kata/ wadi na matawi/ wajumbe wa kamati za uongozi za kila shina na wajumbe wa kamati za utekelezaji za kila tawi na kata kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa kata/wadi wakati wa uchaguzi. Pia, Ibara ya 60 (1) (T) imeongezwa kwa madhu[1]muni ya kupiga kura za maoni ili kuwawezesha wajumbe wote wa kamati ya siasa ya kata/wadi na matawi, wajumbe wa kamati za uongozi za kila shina na wajumbe wa kamati za utekelezaji za kila tawi na kata kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo wakati wa uchaguzi.

Habari Zifananazo

Back to top button