CCM yataka bandari za uvuvi Unguja, Pemba

ZANZIBAR : CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaielekeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujenga bandari mbili kubwa za uvuvi Ngalawa, Unguja na Shumba Mjini, Pemba. Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-2030, uvuvi utaendelea kuwa sekta ya kipaumbele katika kuongeza ajira na kukuza uchumi.

Ilani imeeleza SMZ pia itaelekezwa kujenga masoko makubwa mawili Mkoani na Fungurefu pamoja na masoko madogo matano ya uvuvi. Pia, serikali hiyo itanunua meli kubwa ya uvuvi wa bahari kuu na kujenga viwanda vya kuchakata samaki Shumbamjini, Pemba.

Mikakati mingine
CCM imesema SMZ itaongeza uzalishaji wa samaki kutoka tani 80,085 mwaka 2023 kufikia wastani wa tani 160,000 mwaka 2030. Aidha, itaweka mamlaka ya kusimamia ubora na viwango vya mazao ya baharini, kuanzisha chuo cha uvuvi, pamoja na mamlaka ya kusimamia rasilimali na uhifadhi wa bahari.

Ilani hiyo pia imeeleza serikali hiyo itajenga mabwawa ya kufugia samaki, vizimba baharini na vitotoleshi sambamba na kuanzisha mfumo wa kudhibiti uvuvi usio rasmi. SOMA: Uwanja wa kisasa wakamilika Zanzibar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button