CCM yavuna wanachama wapya Lindi

LINDI: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuvuna wanachama wapya katika mkoa wa Lindi ndani ya wilaya mbili ambao wamelezwa kutoka katika Chama cha Wananchi (CUF).

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla wakati akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Kilwa Aprili 10 na Liwale Aprili 11,2025 mkoani Lindi aliwapokea wanachama hao wapya waliorudisha kadi na kujiunga na CCM.

Aidha, katika Wilaya ya Kilwa zaidi ya wanachama wapya 70 wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia tiketi CUF, Vedasto Ngombale walipokelewa wakieleza kuwa sababu kubwa ya wao kuhamia CCM ni kuridhishwa na utekelezaji wa ilani yao pamoja na maendeleo na mabadiliko lukiluki yaliyofanywa na CCM.

Advertisement

Makalla amewapongeza wanachama hao wapya kwa kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM wanachama na kuutaka uongozi wa CCM katika ngazi ya Wilaya na Mkoa wa Lindi kwa ujumla kuhakikisha wanafanya utaratibu wa kuwapatia kadi wanachama hao ili kukamilisha taratibu na kuwa wanchama kamili.

“Tumewapokea hapa aliyekuwa Mbunge ndugu yangu amerudi CCM na wenzake hapa ilibidi wawe 70 kanini wameongezeka na kuwa zaidi ya 70 ninawaelekeza katibu wa wilaya na mkuu tengenezeni utaratibu wa kuwapatia kadi hawa wanachama wapya,” amesema Makalla.

Ameongeza: “Hili ni jeshi kubwa linalokuja kuongeza ushindi kwa Chama Cha mapinduzi, wengine baada ya kunikabidhi kadi wamenipa na mihuri kabisa maana yake wamefunga ofisi katibu utaiangalia hii mihuri tuweke kwenye kumbukumbu zetu.

Amewataka CCM katika mkoa huo wawatumie vizuri katika wilaya hiyo, na kusisitiza kuwa Ngombale na wenzake bado wananguvu kama walivyoeleza, hivyo wawatumie vizuri kwa manufaa ya chama.

Katika hatua nyingine ndani ya wilaya ya Liwale walikuwa ni wanachama wawili ambao waliwahi kugombea katika uchaguzi uliopita na kupitia tiketi ya CUF Hamis Kilaya na Shaban Kimbinga.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *