DAR ES SALAAM: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM- NEC), CPA Amos Makalla amesema CCM inaendelea kupokea wanachama kutoka katika vyama vya upinzani baada ya kishindo cha ufunguzi wa kampeni.
Pia amesisitiza kuwa kishindo walichoanza nacho watamaliza nacho huku akiongez akuwa wanataka ushindi wa kishindo kwani chama hicho hakicheki na mtu katika kushika dola.
Makalla ameeleza hayo leo Novemba 23,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka.
“Taarifa nilizonazo mpaka nafika hapa kampeni za CCM zinaendelea vizuri lakini pia kupitia uzinduzi na kampeni zinazoendelea maelfu ya wapinzani wanajiunga na CCM,”amesema Makalla.