Chalamila: ‘Mliochukua pesa rudisheni’

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesitisha uzinduzi wa soko la Zakhem lililopo Mbagala, baada ya kubaini wapo madalali waliochukua fedha za watu kwa ajili ya kuwauzia vizimba.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Zakhem loe Agosti 29, 2023  Chalamila amewataka madalali wote waliochukua fedha kuhakikisha wanazirudisha.

Amebainisha kuwa soko hilo ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya sh  bilioni 2,  lina maduka 150, lakini wafanyabiashara waliotuma maombi ni zaidi ya 2,000

Aidha, Chalamila amepiga marufuku  machinga kuuzia bidhaa zao katika barabara iendayo haraka ujenzi wake unaoendelea maeneo ya Mbagala

“Hii barabara iendayo kwa kasi ambayo leo vijana wetu wanatumia kuuza bidhaa zao pale barabarani, naomba leo nitangaze tunawapenda sana lakini sio kuuzia pale barabarani, leo basi likipotea pale mtaanza kusema Mkuu wa Mkoa mzembe…

” Mkuu wa wilaya mzembe msiende kupanga barabara ile sio barabara ya wafanyabiashara holela ni barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi hapa Mbagala….;   “Hii barabara mnayoiona ni awamu ya pili ya ujenzi ambayo mzunguko wake wote unahitaji mabasi 775 ya mwendo kasi na hii barabara imetumia si chini ya Sh.bilioni 217.”amesema.

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button