KONGO : SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo itapokea shehena ya kwanza ya dozi takribani 100,000 za chanjo ya Ugonjwa wa homa ya nyani Mpox.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Wizara ya Afya imesema zoezi la utoaji wa chanjo utaanza kutolewa mwishoni mwa wiki hii .
Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC, kimesema chanjo zingine laki 200,000 zinataraji kuingia nchini Kongo kabla ya mwisho wa wiki hii.
Seŕikali ya Kongo imepokea chanjo hizi kutoka kampuni ya dawa ya Bavarian Nordic iliyoko nchini Denmark.
SOMA : Afrika kunufaika na chanjo Mpox
Mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 17,500 wamethibitika nchini Kongo kuwa wamepata virusi vya homa ya nyani Mpox huku wengine 629 wakipoteza maisha kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO.
SOMA : WHO : Afrika inaweza kutokomeza Mpox ndani ya miezi sita