Charles Hilary kuagwa Mapinduzi Square Zanzibar

ZANZIBAR; Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu, Rajab Ali Ramadhan, akiambatana na Maafisa mbalimbali wa Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, amekagua eneo la Mapinduzi Square, Kisonge, Mkoa wa Mjini Magharibi, kwa ajili ya maandalizi ya shughuli ya kumuaga Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Charles Martin Hilary, aliyefariki dunia Mei 11, 2025 jijini Dar es Salaam.

“Kutokana na mabadiliko ya ratiba, marehemu Charles Martin Hilary ataagwa tarehe 14 Mei 2025 katika Viwanja vya Mapinduzi Square (Kisonge), badala ya Ukumbi wa Idris-Abdulwakil,” imesema taarifa ya Idara ya Mawasiliano Ikulu.

Taarifa imeeleza kuwa mwili yapokelewa leo saa 11:30 jioni katika Bandari ya Malindi, Zanzibar na kuzikwa tkesho saa 10 alasiri makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button