Chelsea yageukia kwa Alejandro Garnacho

Winga wa Manchester United na Argentina, Alejandro Garnacho.

TETESI za usajili zinasema Chelsea inatafakari kumsajili winga wa Manchester United raia wa Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye umri wa miaka 20, baada ya Napoli kusitisha mpango wa kumsajili. (Sky Sports)

Manchester City imeonesha nia kumsajili beki wa pembeni wa Italia, Andrea Cambiaso, mwenye umri wa miaka 24, lakini Juventus itahitaji ada ya karibu pauni milioni 54.8. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Borussia Dortmund imejiondoa kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27, kutokana na mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki wa mchezaji huyo wa Mnchester United kuwa kikwazo. (Mail)

Advertisement

Beki wa kushoto wa Arsenal na Ukraine, Oleksandr Zinchenko, mwenye umri wa miaka 28, anatarajiwa kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho la Januari kufungwa, huku Borussia Dortmund ikilenga kufanikisha mkataba. (Telegraph)

Borussia Dortmund pia inamtupia jicho beki wa kushoto wa Chelsea, Ben Chilwell, mwenye umri wa miaka 28, kama chaguo mbadala. (Sun)