Christian Bella aachia albamu

MSANII wa Muziki wa Dansi kutokea nchini DR Congo, Christian Bella ameachia albamu yake inavyoitwa ‘Rhumba Volume One’ yenye nyimbo 6 alizoimba na bendi yake ya Malaika Bandi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Christian Bella amesema albamu hiyo ameandaa kwa lengo la kurudisha na kuupa heshima muziki wa dansi.
“Albamu ya Rhumba Volume One inanyimbo nzuri na leo nimeachia rasmi ipo kwenye platform zote unaweza kusikiliza kusikiliza na kufurahia muziki wa Rhumba wa aina yake.
“Kubwa ni kurudisha muziki wa Rhumba kwenye hadhi yake ilivyokuwa ikifanya vizuri awali kwa kuwafikia mashabiki na vizazi vyote vilivyopo kufurahia muziki huo.
“Nimefanya albamu mbili Rhumba Volume One na two ambayo zote zina nyimbo 6 ujumla 12 ambapo ya kwanza nimefanya na bendi yangu ya Malaika Band na albamu ya pili nimeimba na wasanii mbalimbali wakiwemo wa Bongo fleva pamoja na hip hop.”amesema
Bella ambaye hivi karibuni aliachia albamu yake inayoitwa ‘Utaniuwa’ inayofanya vizuri katika YouTube na amesema kuwa hali ya muziki imebadilika kwa sasa watu wanaangalia matokeo na mauzo ya kazi uliyofanya.
Pia ameongeza kuwa lengo la kufanya kazi na wasanii wa Bongo fleva, Hip hop na Taarabu ni kutaka kuwateka mashabiki wa muziki hiyo ilikuupenda zaidi muziki wa Dansi.