Chunya waanza kung’ata walioshindwa kurejesha mikopo

MBEYA; Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya vikundi vilivyoshindwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa bila riba, ikiwemo kuvifikisha mahakamani na kuweka vikwazo vya kiuchumi katika kata ambako vikundi hivyo vinatoka.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Tamim Kambona, amesema halmashauri imeweka vikwazo ya kutozipatia mikopo kata hizo, ikiwa ni adhabu ili kuhakikisha zinatekeleza wajibu wa kurejesha mikopo.

“Vikundi vingine tutavifikishwa mahakamani kwa kujipatia fedha hizo kwa njia za udanganyifu,lengo letu tunataka wananchi wanufaike na fedha hizi,”amesema Kambona.

Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chunya, Ester Kondobole, amesema hadi sasa halmashauri inadai zaidi ya Sh milioni 600 kutoka vikundi 87 kati ya vikundi 216 vilivyokopeshwa fedha hizo.

Amesema miongoni mwa kata zilizowekewa vikwazo vya kiuchumi kutokana na kutorejeshwa kwa mikopo hiyo ni Makongorosi, Chokaa na Mamba.

Kondobole amelitaja kundi la watu wenye ulemavu kuwa miongoni mwa makundi yenye changamoto katika urejeshaji wa mikopo kwa wakati.

Ameongeza kuwa changamoto hiyo pia imeonekana katika vikundi vya vijana, ambao baadhi yao huchukua mikopo na kushindwa kutejesha huku wengi wao wakihama katika maeneo yao baada ya kupata mikopo

Amesema changamoto hiyo ianachangiwa na kuwa vijana wengi katika halmashauri hiyo wanaojishughulisha na uchimbaji, ambapo hali ya shughuli hizo kuwafanya kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button