Chuo cha Nyerere chajivunia mifumo bora Tehama

DAR ES SALAAM: Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kimeboresha mifumo ya Tehama ambayo itasaidia kufundisha kwa njia ya mtandao ndani na nje ya chuo.

Akizungumza leo Machi 16, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo, Prof. Haruni Mapesa amesema wameboresha mifumo yote ambapo kupitia mfumo wa ‘smart board’ wanafunzi watajifunza bila ya kuonana na mwalimu na kutuma maswali walimu kulijibu papo hapo au baadaye.

Amesema wameboresha pia mfumo wa kisasa wa ‘Academic Record Manangement System, mfumo ambao utasaidia kuweka rekodi za wanafunzi na  mienendo yao ya kielimu hapo shule hadi kufikia kumaliza bila ya hata kudaiwa kwakuwa mfumo utakuwa unasoma kila kitu.

Mapesa amesema pia kuboresha mfumo wa kisasa wa ‘E-Learning’ utasaidia kuongeza wanafunzi wanaosoma nje ya chuo.

Amesema hata hivyo wamepata mafanikio makubwa ya ufauru, ambapo kwa mwaka 2024/ 2025 wameweza kufanya udahili wanafunzi 6687 wawa na asilimia 17.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button