Coastal vs Kagera: Patashika Ligi Kuu leo

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Arusha na Mbeya.

‘Wagosi wa kaya’ Coastal Union itakuwa mwenye wa ‘walima miwa’ Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Coastal ipo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 8 baada ya michezo tisa wakati Kagera Sugar ni ya 14 ikiwa pointi 5 baada ya michezo nane.

Advertisement

SOMA: Coastal yakimbia Dar, yahamia Arusha

Katika mchezo mwingine ‘Walima zabibu’ Dodoma Jiji itakuwa mgeni wa ‘wachimba dhahabu’ wa Chunya, Ken Gold katika uwanja Sokoine jijini Mbeya.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya saba ikiwa pointi 12 baada ya michezo tisa wakati Ken Gold ni ya 16 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 4.

Mchezo kati ya Simba na JKT Tanzania uliokuwa ufanyika leo umeahirishwa kutokana na baadhi ya wachezaji wa JKT kuwa na majeraha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka wakati wakitoka Dodoma kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.