Daaah Twaha Kiduku mwoga wa sindano!

BONDIA Twaha Kasim ‘Twaha Kiduku’, haogopi ngumi za mabondia wenzake anaokutana nao ulingoni, lakini anasema anaogopa kitu kimoja tu, nacho ni kuchoma sindano akienda hospitalini.

Hata hivyo amewashauri mabondia wenzake kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara, ili wajitanmbue vyema kwa kuwa masumbwi ni kazi inayowaingizia kipato, hivyo wanapaswaa kuwa na afya bora siku zote.

Advertisement

“ Kuchoma sindano daaah ni mtihani sana …ni kitu ninachokiogopa lakini nina mshukuru Mwenyezi Mungu nimepima vizuri na sasa ninawaambia Tanzania kwa ujumla tukutane Mwanza Julai 29, ”amesema Kiduku muda mfupi baada ya kumaliza tukio la kupima afya ikiwa ni maandalizi ya pambano hilo.

Kiduku na mpinzani wake, Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini wanawania mkanda wa ubingwa wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Duniani (WBF) katika pambano litakaofanyika Julai 29, mwaka huu (2023) jijini Mwanza.

/* */