Dar watakiwa kutumia fursa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kukuza kipato na kuimarisha uchumi kupitia fursa zitakazopatikana kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Mkutano huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unatarajia kufanyika kuanzia Julai 25 hadi 26, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo, Julai 21, 2023 katika mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa JNICC.

Advertisement

“Tutakuwa na wageni wasiopungua 1200, ambao watakula, watalala na watatembelea maeneo mbalimbali,” amesema Chalamila na kueleza kuwa wageni hao wanatarajia kuanza kuwasili Dar es Salaam kesho Jumamosi Julai 22.

Amesema zaidi ya hoteli 40 zitatumika na wageni hao, hivyo mkutano huu pia ni fursa ya kutangaza utalii wa nchi na wamejiandaa kutangaza bidhaa zilizopo nchini kupitia mabanda ya wafanyabiashara.

“Ushiriki wa wafanyabiashara ambao tumewaleta hapa watakuwa zaidi ya 100 na wamekwisha andaliwa vizuri kuhusiana na bidhaa, aina ya bidhaa, uzzaji wao kwa ujumla pia kujali wateja ‘customer care’ na kujiunga na maandalizi haya hakuhitaji gharama zozote,” amesema Chalamila

Hata hivyo, Chalamila amesema mkutano huu ni matunda ya juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi na kuwa kiongozi wa kutangaza utalii wa nchi ikiwemo utalii wa mikutano hivyo fursa mbalimbali zinaendelea kufunguka nchini.

8 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *