DC Ileje asisitiza uwajibikaji malezi kwa watoto

SONGWE: Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, leo Machi 26, 2026 ameongoza tukio la Siku ya Afya na Lishe katika kijiji cha Isongole, likilenga kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu afya bora na lishe sahihi.
Katika tukio hilo, wakina mama walipata elimu ya afya na lishe kutoka kwa wataalamu wa afya, huku watoto wakipata fursa ya kupimwa afya zao.

Jumla ya watoto 104 walipimwa, ambapo watoto 26 walibainika kuwa na udumavu, 2 uzito pungufu, 1 uzito uliozidi na 1 ukondefu.
Akizungumza katika tukio hilo, Mgomi alisisitiza umuhimu wa wazazi, hususan kina mama, kufuatilia kwa karibu afya za watoto wao ili kuhakikisha wanakua katika hali bora.

Aidha, aliwahimiza kina baba kushiriki kikamilifu katika malezi na kulea watoto kwa ushirikiano, badala ya kuwaachia kina mama jukumu hilo peke yao.




Start making cash right now… Get more time with your family by doing jobs that only require for you to have a computer and an internet access and you can have that at your home. Starvt bringing up to $18012 a month. I’ve started this job and I’ve never been happier and now I am sharing it with you, so you can try it too. You can check it out here…
HERE→→→→→ https://PayAtHome1.Com/