DC Munkunda ampongeza Rais Samia fedha za miradi Mwanga

KILIMANJARO: Akiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Wilaya ya Mwanga, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahamisi Munkunda amemshukuru Rais Samia Suhulu Hassan kwa uwezeshaji fedha za miradi wilayani humo.

Pongezi hizo pia zimeelekezwa kwa Waziri wa Tamisemi, Mohammed Mchengerwa kwa miongozo na uongozi makini uliofanikisha uendeshaji wa mabaraza kwa ufanisi.
“Pongezi pia kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa usimamamizi, na ushauriano mzuri wa karibu,” amesema DC Mwanahamisi.

Rais Samia afanya uteuzi wakuu wa wilaya, wakurugenzi

 

Katika ujumbe huo wa pongezi kwa viongozi hao, DC Mwanahamisi ameahidi kushirikiana na kuendeleza mafanikio kwa mustakabali wa wananchi wa Mwanga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button