Deni la serikali lafikia Sh tril.71

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema mpaka kufikia Juni 30, 2022 deni la serikali lilikuwa Sh tril 71.
31 ikilinganishwa na Sh tril 64.
52 mwaka 2020/2021, ikiwa ni ongezekezo la Sh tril 6.79 sawa na asilimia 10. 5 ikilinganisha na Sh tril 7.79 sawa na asilimia 13.7 kwa mwaka uliopita.
–
CAG Kichere amesema hayo leo Machi 29, 2023 wakati akitoa taarifa kuhusu uwasilishaji wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni, 2022 katika Ikulu ya Dar es Salaam.
–
Akiwasilisha taarifa hiyo, CAG Kichere amesema kuwa deni la ndani limefikia Sh tril 24.04 na deni la nje Sh tril 47.27 kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Mwaka wa fedha 2020/ 2021 deni la ndani lilikuwa Sh tril 18.93 ndani na nje Sh tril 45.79.