Diaspora kushiriki maoni Dira ya Maendeleo 2050

RAIS Samia Suluhu amewataka Wananchi wote pamoja na wale wanaoishi Ughaibuni (DIASPORA) kushiriki kikamilifu katika uandishi wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Kiongozi huyo wa nchi amesema hayo leo katika sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Amesema wao binafsi au kupitia makundi yao watashiriki zoezi hilo kupitia njia za kisasa zitakazoanishwa na Tume ya Mipango hapo baadaye.

“Baada ya kukamilisha uandishi wa dira ijayo, tume iandae makala fupi ya dira hiyo ambayo itakuwa na lugha rahisi inayoeleweka kwa raia weng.” Amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button