RASIMU ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ilizinduliwa Desemba 11, 2024 na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi baada ya maoni kukusanywa kutoka kwa wananchi na wadau wa maendeleo milioni 1.17.
Miongoni mwa malengo ya dira hiyo hadi 2050, ni Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ngazi ya juu yenye uchumi mseto, stahimilivu, imara na jumuishi pamoja na kutokomeza aina zote za umasikini, hususani kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, sambamba na kuimarisha maendeleo sawia kimkoa.
Kipengele kinachoangaziwa leo katika rasimu hiyo ya dira ni ubunifu wa vyanzo mseto vya fedha na matarajio yake pamoja na uwiano endelevu wa mapato na matumizi pamoja na matarajio yake: Rasimu ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2050 imeeleza kuwa Tanzania inapaswa kubuni na kuibua vyanzo vipya vya mapato kukidhi mahitaji ya maendeleo.
Imevitaja vyanzo vipya ni pamoja na masoko ya fedha na mitaji, ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi, uhisani wa kibinadamu. Imeeleza kuwa ugharimiaji wa maendeleo Tanzania kwa sasa unategemea vyanzo vya mapato mbalimbali, vikiwemo kodi, ushuru na tozo, mikopo ya ndani na nje, uwekezaji wa kigeni, mikopo na misaada.
Rasimu hiyo imeeleza kuwa Tanzania inatekeleza mipango mbalimbali ya kuimarisha vyanzo anuai vya mapato, ikiwemo Soko la fedha na Mitaji la Dar es Salaam na mifumo yake. Pia, Tanzania imeanzisha kituo cha ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi kwa ajili ya kukuza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi.
Benki Kuu ya Tanzania (Bot) imekuwa ikiboresha masoko ya kifedha kwa kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na miundombinu bora ya soko la fedha, kuweka sheria zinazofaa na kuwezesha maendeleo ya ubunifu wa fedha na zana za soko la mitaji.
Rasimu imeeleza kuwa ni vyema Tanzania ikachukua hatua endelevu za kuongeza soko la fedha na mitaji kwa sababu ni muhimu katika kukabiliana kwa kutumia ufanisi kutatua changamoto ikiwemo mapokeo duni ya dhana ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi.
Changamoto nyingine ni kwamba soko la fedha ni dogo na linakwepa vihatarishi, wakati soko la mitaji bado liko katika hatua za awali na kukosa nguvu ya mabadiliko.
Matarajio ya Rasimu ifikapo 2050 katika ubunifu wa vyanzo mseto vya fedha ni kuongezeka kwa matumizi thabiti ya mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi kama njia ya kugharimia na kuendeleza miradi ya maendeleo.
Inatarajia kuwa na soko la fedha na mitaji lenye ubunifu, ufanisi na tija, lililojengwa juu ya misingi wezeshi ya kisheria inayozingatia uwazi, usawa, uwajibikaji na upatikanaji wa taarifa sahihi kwa washiriki wote.
Pia, inatarajia kuwa na mifumo ya mitaji jumuishi inayolenga kuwezesha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kuwa na jamii ya wajasiriamali imara yenye mtazamo wa uthubutu na nidhamu ya kuchukua mikopo kama njia ya kupata mitaji ya miradi ya maendeleo.
Aidha, inatarajia kuwa na mfumo thabiti wa ikolojia ya vyanzo mbadala vya fedha na mitaji kama vile mitaji binafsi.
Uwiano endelevu wa mapato na matumizi Rasimu ya Dira 2050 inaeleza kuwa uwiano wa mapato na matumizi ni hali ambayo serikali inakuwa na uwezo wa kudhibiti mapato na matumizi na deni la taifa bila kuongeza mzigo wa kifedha na deni la taifa au kuathiri ukuaji wa uchumi wa muda mrefu.
Inaeleza kuwa kipindi cha miongo miwili iliyopita, Tanzania imefanya mageuzi mbalimbali yenye lengo la kuimarisha uwezo wake wa kifedha na kuboresha usimamizi wa matumizi. Hatua hizo ni pamoja na kupanua wigo wa kodi, kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kutumia teknolojia za kidijiti, kuboresha uwazi na elimu kwa mlipakodi, usimamizi wa matumizi na ukaguzi.
Inabainisha kuwa msingi wa kujenga uchumi imara na wenye ushindani unajumuisha mikakati ya kuboresha usimamizi wa bajeti, kupunguza nakisi ya bajeti na kuhakikisha kuwa serikali inakidhi mahitaji yake ya kifedha kwa ajili ya ukuaji wa uchumi endelevu.
Rasimu inaeleza kuwa pamoja na mafanikio hayo, wigo wa kodi umebaki kuwa finyu, wenye ufanisi mdogo na uwiano wa kodi na pato la taifa wa kiwango cha chini ikilinganishwa na nchi zenye uchumi unaolingana na Tanzania.
Inaeleza kuwa usimamizi wa kodi umethiriwa kwa kiwango kikubwa na mazingira ya biashara yasiyo rafiki baina ya mlipa kodi na mamlaka za ukusanyaji kodi. Aidha, ongezeko la matumizi ya serikali limesababisha kuongezeka kwa ukopaji huku mikakati ya usimamizi wa madeni ikipunguza uwezekano wa sekta binafsi kupata mikopo.
Vilevile, uboreshaji katika usimamizi wa matumizi ya serikali umeimarisha utoaji wa taarifa na usimamizi pasipokuboresha mfumo wa kuweka vipaumbele vya kimakakati.
Aidha, rasimu hiyo inaeleza kuwa, usimamizi wa deni la taifa ni muhimu katika kuhakikisha uendelevu wa uwiano wa mapato na matumizi ya kifedha. Suala ambalo linahitaji uwajibikaji na uwazi, pamoja na usimamizi bora wa uwekezaji. Kwa sasa, deni la taifa linatajwa kuwa stahimilivu.
Dira ya 2050 inatarajia kutakuwa na mfumo wa kodi wenye usawa, ufanisi na tija, unaoboresha uwiano kati ya kodi na pato la taifa, na kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo, mfumo wa kikodi wenye uwazi na unaotabirika,
unaowezesha kuanzisha, kukuza na kurasimisha biashara, ili kutoa fursa za ajira na kupanua wigo wa walipa kodi.
Pia, inatarajia kuwepo usimamizi thabithi wa deni la taifa na kuhakikisha linakuwa himilivu na endelevu na mgawanyo bora wa rasilimali bora wa rasilimali za taifa, usimamizi thabiti wa bajeti unazingatia vipaumbele vya taifa na thamani ya fedha katika matumizi ya serikali.
Aidha, inatarajia mipango ya bajeti inayohakikisha uwiano wenye tija baina ya uwekezaji kwa ajili ukuaji wa baadaye, na matumizi ya kawaida kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa sasa.
I was recommended this blog through my cousin. I am no longer certain whether
or not this post is written through him as nobody else
realize such targeted approximately my trouble.
You are incredible! Thank you!