Biteko azindua mfuko kukabili magonjwa ya mlipuko

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko amezindua mradi wa Mfuko wa Kukabiliana na Magonjwa ya Mlipuko, utakaogharimu zaidi ya Sh billioni 90, huku akizitaka sekta zote zitakazoshiriki katika utekelezaji wake kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Ni mradi wa miaka mitatu unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), la Chakula na Kilimo (FAO), na la Watoto Duniani (UNICEF), kwa lengo la kuimarisha uwezo wa kuzuia, kujiandaa, kukabiliana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko na dharura.
“Mradi huu una manufaa makubwa, hivyo sekta za serikali ikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinapaswa kutekeleza kwa uaminifu mkubwa. Serikali itashirikiana na wadau wa ndani na nje ya Tanzania kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama katika sekta ya afya” amesema.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe, amesistiza umuhimu wa idara husika kusimamia mradi huo ipasavyo, kwa kujikita zaidi kudhibiti magonjwa ya mlipuko hasa katika maeneo yenye mikusanyko ya watu, ikiwemo vituo vya mabasi, sokoni, viwanja vya ndege na mipakani.
Amesema mradi utasaidia kuimarisha uwezo wa kukinga, kugundua nakudhibiti magonjwa yote ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya dharura vya kuhifadhi wagonjwa.
“Tutaimarisha pia mifumo ya upatikanaji maji safi na salama, upatikanaji wa taarifa kwa haraka kuanzia ngazi ya jamii mpaka mkoa, pamoja na maabara zetu kuwa na uwezo wa kufanya vipimo kwa haraka na kutoa matokeo sahihi,” amesema.
I get paid more than $100 to $500 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily 💵$20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
Here is I started.→→→→→→→→→ https://Www.Works6.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com