Dk Chana: Ajenda uhifadhi mazingira zidumu

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amezitaka serikali za vijiji kuweka ajenda ya uhifadhi wa mazingira na kudhibiti moto ziwe za kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

Dk Chana amesema hayo leo Oktoba 2, alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Mponda, wilayani ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

“Utunzaji mazingira ni pamoja na kupanda miti, hivyo ni lazima tupande miti na tunaposafisha mashamba tuwe makini na matumizi ya moto,” Dk Chana amesema.

SOMA: Dk Chana afungua sekondari Josephat Kandege

Aidha, ameendelea kuhamasisha wananchi kuwa na mizinga ya nyuki ili kupata asali itakayowasaidia kujiinua kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Chana amewataka wananchi kuacha kuingiza mifugo hifadhini ili kuepukana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Naye, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii (anayeshughulikia maliasili) Kamishna Benedict Wakulyamba amewapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kulinda shamba la Miti Mbizi na kuwahimiza kuendelea kulinda misitu.

Waziri Chana yuko mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Habari Zifananazo

Back to top button