Dk Gwajima ataka wanawake kutumia nishati safi kupikia

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme ili kulinda afya za familia, mazingira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
Dk Gwajima ametoa wito huo wakati akizungumza katika Kongamano la Pili la Wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lililofanyika Dar es Salaam, lenye lengo la kuhamasisha Dk Gwajima ataka wanawake kuhamasisha nishati safi kupikia Geita yakamilisha michoro 2, ramani 15 za mipango miji Serikali yaombwa bajeti kutekeleza kilimo ikolojia hai ORD320601 matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme.
Amesema kongamano hilo limefanyika wakati dunia ikielekea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026 yenye Kaulimbiu: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana; Msingi Jumuishi wa Kufikia Dira ya Taifa 2050”.
Kwa mujibu wa waziri huyo, kaulimbiu hiyo inasisitiza umuhimu wa uwezeshaji wanawake na usawa wa kijinsia katika kufanikisha maendeleo ya taifa, ikiwemo katika sekta ya nishati ambayo ni moja ya nguzo muhimu za maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Amesema takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonesha takribani asilimia 81.5 ya kaya nchini bado zinatumia kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia, kuni zikichangia asilimia 55.5 na mkaa asilimia 26. SOMA: Asilimia 80 nishati safi fursa kiuchumi
Amefafanua kuwa ni asilimia 18.5 ya kaya zinazotumia nishati safi ya kupikia, zikiwemo gesi asilimia 9.4, umeme asilimia 4.3 na nishati nyingine asilimia 4.8, hali inayoonesha bado kuna kazi kubwa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.
Amesema serikali imeweka ajenda ya nishati safi ya kupikia kama kipaumbele cha kitaifa kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024 hadi 2034. Lengo la mkakati huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia huku matumizi ya umeme yakilenga kufikia angalau asilimia 20.
Dk Gwajima alisema wanawake wamekuwa waathirika wakubwa wa matumizi ya nishati zisizo safi kwa sababu ya athari za kiafya zinazotokana na moshi pamoja na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Amesema changamoto kubwa kwa sasa si upatikanaji wa umeme, bali ni uhamasishaji wa jamii kuutumia kama nishati ya kupikia huku akieleza kuwa watu wengi bado wana dhana potofu kwamba kupika kwa umeme ni gharama kubwa.
Amesema maendeleo ya teknolojia yamewezesha kutengenezwa kwa majiko ya umeme yanayotumia umeme kidogo ambapo baadhi yanaweza kupika mlo kwa kutumia chini ya uniti moja ya umeme ya thamani ya chini ya Sh 350. “Gharama ya kupikia kwa umeme inaweza kuwa ndogo ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa ambayo siyo tu yanaharibu mazingira, bali pia yana athari kubwa kwa afya ya watumiaji,” alisema.
Pia, amesema Tanesco imeendelea kutekeleza programu za kuongeza matumizi ya umeme katika kupikia, ikiwemo mradi unaofadhiliwa na Taasisi ya MECS unaowawezesha wafanyakazi kukopeshwa majiko na kulipa kidogo kidogo kupitia makato ya mishahara.
Pia, ametaja mpango wa On Bill Financing (OBF) unaowawezesha wateja wapya wa Tanesco kuunganishiwa umeme na kukopeshwa majiko, wakifanya malipo ya gharama hizo kupitia manunuzi yao ya umeme.



