Makamu wa Rais Dk Philip Mpango kwa niaba ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Shirikisho la Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kati (ACEAC) linalojumuisha nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhashamu Askofu José Moko.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha mzungumzo hayo yalilenga kujadili namna ya kutafuta amani katika mgogoro unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.