Dk Mwinyi kumwakilisha Rais Samia mkutano SADC

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Novemba 20, 2024 Harare nchini Zimbabwe.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 18, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa pamoja na hayo, Rais Dk Mwinyi ataongoza Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi za Siasa, Ulinzi na Usalama unaotarajiwa kufanyika siku hiyo hiyo.

Mkutano huo utajadili masuala ya amani na usalama katika ukanda wa SADC na masuala mengine ya kuimarisha mtangamano.

Advertisement