RC Simiyu: Tuongeze uzalishaji, tuweke akiba ya chakula

WAKAZI wa Mkoa wa Simiyu, wametakiwa kuongeza nguvu katika kilimo na uzalishaji wa mazao ya chakula na kuweka akiba ya chakula.

Wito huo ulitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Chakula Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka kuanzia Oktoba 16, ambapo mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani Simiyu kuanzia leo.

Alisema maadhimisho hayo yatatoa fursa kwa wakazi wa mkoa huo kuonesha bidhaa za chakula wanazozalisha na kutumia, pia watapata fursa ya kujifunza mbinu mpya za uzalishaji wa kisasa.

Advertisement

“Tumelenga kuhakikisha wakazi wa Mkoa wa Simiyu, wanaopata elimu hii ya uzalishaji, utunzaji na uhifadhi wa chakula na pia kupambana na magonjwa,” alisema.