Dk Samia kuhitimisha kampeni Mwanza

MWANZA: MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufunga kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2025 mkoani Mwanza.
Katibu CCM Mkoa, Omary Mtuwa, ametoa taarifa hiyo leo Oktoba 26, na kwamba shughuli hiyo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba, wilayani Ilemela, ambapo maandalizi yote yamekamilika.
“Tunawakaribisha wananchi wote, wanachama wetu na wasiokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,” amesema na kuongeza kuwa: CCM imechagua kufungia kampeni mkoani Mwanza kufuatia wingi wa wapiga kura waliopo Kanda ya Ziwa, ambao ni takribani asilimia 38 ya wapiga kura wote nchini, huku Mwanza pekee ikikadiriwa kuwa na wapiga kura takribani milioni mbili”.
Akizumgumzia maendeleo ya kampeni kwa ujumla toka kuanza kwakwe Agosti mwaka huu, Mtuwa amesema zimefanyika salama kwa CCM kufanikiwa kuwafikia wananchi wengi kama ilivyokusudiwa.



