Dk Tulia aendesha zoezi la misaada Mbeya

MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania ameendelea na zoezi la kutoa msaada wa vyakula, mboga na mavazi kwa wananchi wa Mbeya Mjini wanaoishi katika mazingira magumu.

Dk Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, ametoa msaada huo Desemba 21, na kutembelea kata 8 na kukamilisha kata 17 katika kata 36 za Jiji la Mbeya anazotarajia kuzifikia.

Advertisement

Aidha lengo la kufanya hivyo ni kufikisha tabasamu kwa wananchi wake ambao hawajiwezi ili wafurahie katika msimu huu wa sikukuu za Krismass na mwaka mpya.