MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini, Dk Tulia Ackson, amewataka wananchi kuchagua viongozi wenye uwezo wa kushughulika na changamoto zao kwa urahisi.
Dk Tulia amezungumza hayo leo wakati akihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Songwe zilizofanyika katika uwanja wa Uwanja wa Mwaka, Tunduma.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika kesho, ambapo ameongeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama pekee kinachojua changamoto zao na kinao uwezo wa kuzitatua kwakuwa kwa dhamana iliyopewa kupitia Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.