‘Tumieni tafiti kukuza Uchumi wa Buluu’

DAR ES SALAAM; Wadau wa sekta ya bahari nchini Tanzania wamehimizwa kuanza kutumia ubunifu katika tafiti za bahari zilizoboreshwa kwa teknolojia ya kisasa, ili kukuza sekta ya uchumi wa buluu.

Agizo hili limetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, alipokuwa akizungumza na wadau zaidi ya 300 katika Kongamano la Tatu la Kimataifa la Uchumi wa Buluu linaloendelea jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Dk  Biteko amesisitiza umuhimu wa kutumia tafiti za ubunifu zinazokwenda sambamba na teknolojia ya kisasa, ili kuharakisha maendeleo ya sekta ya uchumi wa buluu.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/dk-biteko-afungua-kongamano-uchumi-wa-buluu/

“Tafiti hizi endapo zitafanyika kwa utaalamu na ubunifu zitasaidia katika kuboresha operesheni za uokoaji baharini na kuhakikisha usalama wa maisha ya watu, pamoja na kupunguza ajali za baharini,” alisema Dk Biteko.

Sekta ya uchumi wa buluu inachukuliwa kama mchango muhimu kwa maendeleo endelevu kwa kuzingatia matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na uhifadhi wa mazingira.

“Uchumi wa Buluu unachochea uvumbuzi wa teknolojia ya kibayoteknolojia na nishati mbadala, na kusaidia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” amesisitiza Dk Biteko.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/samia-aelekeza-uendeshaji-uchumi-wa-buluu/

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ametoa ahadi ya serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya uchumi wa buluu, ili kuongeza mtandao wa utaalamu na kukuza maendeleo ya sekta hiyo.

“Serikali imeanzisha Chuo cha Bahari Dar es Salaam kutoa mafunzo kwa mabaharia, manahodha, wahandisi wa vyombo vya majini, na programu zingine zinazohusiana na masuala ya bahari,” amesisitiza Profesa Mbarawa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button