Dogo Yamal awakalisha CR7, King Messi

DAR ES SALAAM: Umeuonaje uwezo wa Lamine Yamal na lile bao lake jana? Sasa rekodi zinaonesha dogo amewapiga bao Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Lionel Messi akiwa na umri wa miaka 17 alicheza michezo 9 tu, alifunga bao 1 na pasi za mabao 0. Cristiano Ronaldo umri wa miaka 17 alicheza michezo 19, mabao 5, pasi za mabao 4.

Lamine Yamal umri wa miaka 17 amecheza michezo 100, mabao 22, pasi za mabao 33.

Pengine Messi na Ronaldo wangepata michezo kwa idadi ya Yamal wangeweza kufikia mabao ya Yamal au hata zaidi, ila unagundua wote wakiwa na umri huo, Yamal ameaminika zaidi ndio maana amecheza michezo mingi.

Lakini pia kwa Barcelona ile Ronaldinho, Patrick Kluivert , Ricardo Quaresma, Javier Saviola kwa wachezaji hawa, Messi angeaminiwa vipi kwa miaka 17, ndio maana alipata mechi chache kwa umri wake.

Kesi ya Cristiano akiwa na umri huo, United ina Diego Forlan, Ole Gunnar Solskjaer, Ruud Van Nistelrooy, Ryan Giggs, halafu ndio umetoka Sporting CP gafla uwaweke hawa benchi au uaminike, lakini hata pale alipocheza ugumu wa ligi yenyewe ni sababu pia.

Hivyo naamini kwa ile Barcelona ya 2003 hadi 2010, Yamal pengine asingeaminika kwa kucheza mechi hizo zote, Barcelona wamepitia kipindi ambacho wanahitaji wachezaji na masuala ya kifedha pia, ndio maana dogo kwa kipaji alichonacho anapata muda zaidi.

Kuna wachezaji pale Barca hawakupata nafasi ya kuaminika ujue unamjua Ibrahim Afellay, unamjua Bojan Krkić, kutoka La Masia acheni nyie.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button