Dulla Makabila aitwa Basata kuhusu wimbo Pita Huku

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata, limemtaka msanii Abdallah Ahmed ‘Dullah Makabila’ kufika katika ofisi za baraza hilo kujadili wimbo wake mpya uitwao Pita Huku, ambao unaendelea kushika nafasi ya kwanza ‘Youtube’.

Taarifa ya kuitwa kwa msanii huyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Basata,  Dk Kedmon Mapana iliyosema: ‘Basata inapenda kuwajulisha kwamba kutakuwa na kikao kitakachofanyika tarehe 21/12/2022 siku ya Jumatano, ajenda ya kikao ni kujadili kuhusiana na wimbo wako wa Pita Huku”.-

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Makabila amethibitisha kupokea barua hiyo: “Nimepokea barua ya wito kutoka Basata, ambayo inahusu wimbo wangu mpya wa Pita Huku, wito nimeupokea na nitafika leo nyie ni walezi wangu katika shughuli zangu za sanaa.-

“Mashabiki zangu asanteni Kwa kuufanya wimbo wetu wa Pita Huku kuwa trending number moja huko mjini Youtube, tuendelee kufuatilia kazi nzuri,”  ameongeza Makabila.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gate token
4 months ago

I am a website designer. Recently, I am designing a website template about gate.io. The boss’s requirements are very strange, which makes me very difficult. I have consulted many websites, and later I discovered your blog, which is the style I hope to need. thank you very much. Would you allow me to use your blog style as a reference? thank you!

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x