EAC yatakiwa kurahisisha usafiri wa anga

JUKWAA la Utalii la Afrika Mashariki (EATP) limezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuondoa vikwazo katika matumizi na kufungua ili kukuza sekta ya utalii katika ukanda na kurahisisha usafiri wa anga.

Katika ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya Utalii ya EAC mjini Bujumbura, Burundi Ijumaa, Mwenyekiti wa EATP, Fred Odek, alisema mikataba ya vizuizi tofauti iliyopo baina ya nchi wanachama ya Huduma za Anga (BASAs) kati ya nchi wanachama ilikuwa ikivuruga uwianishaji wa huduma za usafiri wa anga katika ukanda.

Alitoa mwito kwa nchi wanachama kukamilisha kanuni za EAC ili kurahisisha usafiri wa anga katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na Sekretarieti ya EAC na kulifikia gazeti hili ilisema maonesho hayo yanayohitimishwa Septemba 30, mwaka huu, yalifunguliwa na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Biashara, Uchukuzi, Viwanda na Utalii wa Burundi, Madam Marie Chantal Nijimbere; Waziri wa Masuala ya EAC, Ezechiel Nibigira, Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji katika EAC, Jean Baptiste Havugimana na Meya wa EAC, Bujumbura, Jenerali Jimmy Hatungimana

Alisema kwa kufanya kazi pamoja, nchi wanachama zinaweza kufaidika na usafiri na kukuza sekta ya utalii katika kanda ya EAC.

Kwa mujibu wa Odeh, nauli za ndege katika eneo la Afrika Mashariki zimekuwa juu kutokana na ukosefu wa anga wazi pamoja na ushuru mkubwa unaotozwa na serikali.

Alipongeza mfumo wa Visa ya Mtalii Mmoja wa Afrika Mashariki na matumizi ya vitambulisho vya taifa kama hati za kusafiria katika eneo zima ikiwa ni miongoni mwa sera bora zilizotungwa na EAC.

Kuhusu sekta ya utalii kama moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya fedha za kigeni kwa kanda hiyo, Odek alisema kulingana na upotevu wa Pato la Taifa kwa kanda, utalii wa EAC ulikuwa eneo la pili lililoathiriwa zaidi na janga hilo duniani baada ya Amerika ya Kati.

“Hata hivyo, bado sekta hii ni himilivu na mojawapo ya sekta muhimu zaidi katika kurudisha uchumi wetu kwenye njia ya ukuaji,” alisema.

Akaongeza: “Mwaka wa 2022, tunashuhudia unafuu kwani janga la Covid -19 limekuwa katika masoko yetu mengi muhimu na wasafiri wa kimataifa sasa wana uhakika kamili wa kusafiri. Hata hivyo, wanaofika na mapato bado ni chini ya viwango vya 2019.”

Kuhusu sekta ya ukarimu, alisema pia iliathirika, lakini ilipata nafuu kadiri masharti kuhusu Covid-19 yalivyozidi kuondolewa na kuzifanya nchi wadau kuingia nchini bila sharti la kupimwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Odek aliitaja vita baina ya Ukraine na Urusi imeathiri vibaya watalii wanaowasili Afrika Mashariki hususani katika maeneo kama Zanzibar ambayo nchi hizo zimekuwa vyanzo muhimu vya masoko.

Alibainisha kuwa, vita hiyo pia imeathiri gharama za usafiri wa anga katika eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa gharama za mafuta na bidhaa nyingine.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button