EU kutoa Euro bilioni 4 kuisaidia Misri

BRUSSELS : UMOJA wa Ulaya (EU) umepanga kutoa mkopo wa Euro bilioni 4 kwa ajili ya kuisaidia Misri kukabiliana na changamoto za kifedha.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Brussels, Baraza la Umoja wa Ulaya pamoja na Bunge la Ulaya wanatarajiwa kusaini makubaliano hayo hivi karibuni kabla ya fedha hizo kuanza kutolewa rasmi.
Hatua hii ni sehemu ya msaada mpana uliotangazwa awali na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuiwezesha serikali ya Misri kukidhi mahitaji yake ya kifedha katika kipindi hiki kigumu kiuchumi.
Makubaliano ya awali kuhusu msaada huo yalifikiwa kati ya Baraza la EU, linalowakilisha nchi wanachama, na Bunge la Ulaya, kama sehemu ya ushirikiano endelevu kati ya pande hizo mbili.