Karibu katika page yetu ya urembo na utanashati ambapo tunajifunza jinsi ya kupendeza unapoenda ofisini, kanisani au kwenye shughuli mbalimbali.Leo tunazungumzia vazi la suti ni vazi ambalo unapovaa kuna vitu unapaswa kuzingatia.
Jinsi gani unaweza kutokelezea na suti ni wapi unaenda na kunatukio gani?unapaswa kujua ili kuzingatia rangi unayoenda na na tukio husika. Suti uvaliwa na mtu yoyote Mwanamke au Mwanaume tofauti ni jinsi ya ukataji. Unapovaa Suti unahitaji mchanganyiko wa mtindo, kujiamini, na maelezo madogo yanayofanya uonekane nadhifu na wa hadhi machoni pa watu.
Hapa kuna vidokezo vya msingi:Chagua Suti Sahihi inayokukaa vizuri mwilini
Suti inayotosha vizuri Usivae suti kubwa au ndogo sana. Iwe inakukaa vyema mabegani, kifuani, na kwenye mikono. Itakayokufanya kuwa huru zaidi kuweza kukunja mikono na kunyoosha. Rangi na muundo kwa mwonekano rasmi, chagua rangi kama blue, kijivu, au nyeusi. Kwa hafla zisizo rasmi, unaweza kujaribu suti zenye rangi kama beige, kahawia, au zenye muundo wa mistari (pinstripe).Ili kukamilisha vazi lako Suti nguo kama Shati na Tai ni muhimu sana kwenye mwili wako.
Shati safi na lililopigwa pasi vizuri, Nyeupe ni rangi salama zaidi, lakini pia rangi laini kama light blue, pink, lavender au nyeusi zinafaa.Tai inayolingana Kama suti na shati ni za kawaida, tumia tai yenye rangi au muundo wa kuvutia. Epuka tai pana sana au nyembamba kupita kiasi. Hizo zinapoteza muonekana lazima tai iwe ya wastani kiasi.
Viatu vilivyong’arishwa – Viatu vya Oxford, Derby, au Loafers vinapendeza na suti. Rangi ya viatu inapaswa kulingana na mkanda. Hakikisha unalingana na rangi ya viatu.Viongezeo (Accessories) vya kistaarabu. Saa ya mkononi ni muhimu unaonekana mtu unayezingatia muda na kwenda na wakati zaidi.Saa ya kifahari, si kubwa sana, na yenye muundo wa kistaarabu inakamilisha mwonekano wako.
Unaambiwa kitambaa cha mfukoni kinaongeza haiba, lakini kisiwe na muundo mkali kupita tai. Hereni au pete (kama unapenda) viwe vidogo na visivyopiga kelele sana. Ikiwa ni mchana, miwani ya designer inaweza kuongeza mvuto. Lakini kama unaweza kuvaa miwani ya kawaida inaongeza mwonekano.
Tembea kwa kujiamini, uwe na mgongo ulionyooka na uonekane mtulivu.Tabasamu kidogo na usiwe na mkao wa kujikunyata au kukosa raha. Kaa ikiwezekana kwa kukunja nne au kwa kujiamini zaidi kama mtu ambaye nimavazi yako ya siku zote. Kwa kufuata haya yote, utatokelezea na suti kwa namna ya kuvutia na ya kipekee! SOMA: Mshindi Tamasha la Mavazi Samia akabidhiwa mil 3/-