Flora mbaroni kwa kuuza viwanja vya watu

MWANZA: JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia mwanamke mmoja anayejiita Flora Kasambala ambapo jina halisi anaitwa Bigister Mbowe ,42, kwa kosa la kughushi nyaraka na kuuza viwanja namba 19, 20 kitalu K, vilivyopo katika Mtaa wa Nyakalekwa Kata ya Luchelele wilayani Nyamagana Jijini Mwanza wakati akijua viwanja hivyo sio mali yake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo DCP. Willbroad Mutafungwa, amesema September 06, 2024, Mtuhumiwa Bigister Mbowe aliuza kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 480 kwa Khamis Abdallah ambaye ni Mwandishi wa Habari.

SOMA ZAIDI: Ndondole mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

RPC Mutafungwa amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kutapeli na kuwalaghai watu kwa kuwauzia viwanja ambavyo sio mali yake na kughushi nyaraka za umiliki wa viwanja huku akishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa ambao sio waadilifu wanaotumia nafasi zao kuwaaminisha wanunuzi kwamba maeneo hayo yanamilikiwa kihalali na mtuhumiwa Bigister.

Watuhumiwa wengine katika shauri hilo ni Yohana Petro Kirangi ,45, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakalekwa, Mohamed Amir Omari ,52, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Nyakalekwa, Salome Peter William ,26, Mkazi wa mtaa wa Nyasaka, Benedicto Michael Mathias ,50, Dalali wa viwanja na mkazi wa Buhongwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button