G7 yaahidi kushughulikia usawa wa kiuchumi duniani

CANADA : MAWAZIRI wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Kundi la G7 wamekubaliana kushughulikia changamoto ya ukosefu wa usawa katika uchumi wa dunia, sambamba na kuendeleza mashinikizo dhidi ya Urusi kupitia uwezekano wa kuongeza vikwazo.

Makubaliano hayo yalifikiwa jana katika mkutano uliofanyika katika eneo la mapumziko la mlima la Kananaskis, nchini Canada, ambapo viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu hali ya uchumi wa kimataifa.

Waziri wa Fedha wa Canada, François-Philippe Champagne, amesema kuwa licha ya tofauti zilizokuwapo awali kati ya baadhi ya nchi wanachama, hatimaye walifikia muafaka juu ya masuala muhimu yanayogusa uchumi wa dunia.

“Tumejadili kwa kina na kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu changamoto kubwa zinazoukabili uchumi wa dunia. Kipaumbele kimetolewa kwa hatua za kupunguza pengo la usawa wa kiuchumi kati ya mataifa ya nje na ndani ya nchi,” alisema Champagne.

Katika hatua nyingine,Viongozi hao pia walizungumzia hali ya kisiasa na kiusalama duniani, wakieleza kuwa wanatazama kwa karibu mzozo unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine, na kuwa tayari kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi iwapo hali itaendelea kuzorota.

Mkutano huo wa mawaziri umeandaliwa kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za G7 unaotarajiwa kufanyika Kananaskis kuanzia Juni 15 hadi 17, ambapo Rais wa Marekani Donald Trump, anatarajiwa kuhudhuria.

SOMA: G7 kujadili nishati ya umeme Ukraine

undwa na mataifa saba yenye uchumi mkubwa duniani ambayo ni: Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.

Makubaliano ya viongozi hao yameelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuelekea uchumi jumuishi, unaozingatia maendeleo endelevu na kupunguza pengo kati ya mataifa tajiri na yale yanayoendelea.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button