Gabo Zigamba awatunuku tuzo waigizaji ‘Baraluko’

MWIGIZAJI wa filamu nchini Tanzania, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ ametoa tuzo kwa wasanii wake alioigiza nao tamthilia yake mpya iitwayo “Baraluko”,
Amesema kuwa ni kazi ya kipekee inayobadilisha mwelekeo wa tasnia ya filamu nchini na kutokana na uwezo walioonesha kwenye tamthilia hiyo ameongeza awapongeze kwa juhidi zao.
Akizungumza na HabariLeo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tuzo hizo, Gabo amesema tamthilia hiyo ya kipeke aliyoifanya kwa lengo la kurudisha shukrani kwenye jamii itamfanya kukusanya zaidi mashabiki wake ndani na nje ya Tanzania.
“Nimetoa tuzo hizi kwa kutambua mchango wa wasanii na kazi nzuri waliyoifanya kwa kuwa najuwa wametumia uwezo mkubwa katika kazi ya Baraluko”
SOMA ZAIDI: Gabo Zigamba azindua tamthilia ya Baraluko
“Baraluko inalenga kuonyesha maisha halisi ya Mtanzania na kuhamasisha ufuatiliaji wa kazi za ndani miongoni mwa watazamaji wa Kitanzania,”
“Baraluko inamaana ya mipasuko inayohusiana na Mapenzi na maisha halisi ya watanzania kwamba unakuta biashara ya uzi ameifanya Babu hadijukuu anafanyia biashara hiyo hiyo hawabadilishi,” amesema Gabo
“Jambo lolote ukiweka kwa uangalifu linaweza kuwa zuri. ‘Baraluko’ imeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu na naamini itabadilisha mtazamo wa watu kuhusu tamthilia zetu,” amesema Gabo.
Ameongeza kuwa mara nyingi wasanii wanafanya kazi katika television na kuwasahau mashabiki wao wa Kimataifa.
“Tunalenga kuwafikia mashabiki wetu wote, kuwaburudisha na kuwaelimisha kwa kutumia maisha ya kila siku ya Mtanzania kama msingi wa simulizi na kutuangalia duniani kote kwa kile tunachokifanya .”amesema
Kwa upande wake Zulfa Shoo maarufu kama Zulfa Msomali amesema kuwa anafurahia sana kupata tuzo kama Mwigizaji Bora wa kike nimefurahi kwa tuzo hii.
“Ni tuzo yangu ya kwanza kuwai kupokea awali nilikuwa nikifanyakazi sikuwa nikifikilia kupata tuzo naamini itakuwa tuzo yangu ya kwanza kuleta mabadiliko katika kazi zangu.
Aidha tamthilia hiyo imeweza kuwahusisha na wachezaji wa mpira kutoka Simba na Yanga ilikuongeza Ubunifu na ufanisi katika kufikia Dunia.
Ameongeza kuwa tamthilia hiyo inaangazia zaidi masuala ya mapenzi, na itakuwa ikirushwa kila baada ya siku tano.
Vilevile, timu ya watayarishaji imepanga kufanya ziara katika vyuo vya sanaa ili kuwahamasisha vijana na kushiriki uzoefu wa utendaji wa kazi kwa vitendo.