GABON : KIONGOZI wa Kijeshi nchini Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, ameibuka mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika Jumamosi, akipata zaidi ya asilimia 90 ya kura, kulingana na matokeo ya awali.
Ushindi huu unakuja mwaka mmoja baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomaliza utawala wa familia moja uliojumuisha takriban miaka 60.
Hata hivyo, wakosoaji wanamtuhumu Oligui Nguema kwa kubuni katiba mpya na kanuni za uchaguzi ambazo zimewapa faida, huku baadhi ya vigogo wa upinzani wakitengwa ili kutoleta changamoto katika kinyang’anyiro hicho.
Katika uchaguzi huo, Oligui Nguema, mwenye umri wa miaka 50, alipambana na wagombea saba, akiwemo Waziri Mkuu wa zamani, Alain Claude Bilie-by-Nze, pamoja na vinara wawili wa chama cha zamani cha PDG.
Ushindi huo unaimarisha nafasi yake ya kisiasa, miezi kadhaa baada ya kutekeleza mauaji ya Rais Ali Bongo, ambaye aliongoza nchi hiyo tangu mwaka 1967.