Gavana BoT awaasa wahitimu uadilifu, uzalendo

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amewataka wahitimu wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania kudumisha uadilifu, uzalendo na ubunifu wanapoanza safari zao katika sekta ya fedha.

Akizungumza katika Mahafali ya Nne ya Chuo hicho ambako alikuwa Mgeni Rasmi, Gavana Tutuba amesisitiza kuwa sekta ya fedha ni moyo wa uchumi wa taifa hivyo inahitaji watu wenye maadili makubwa na ujuzi wa hali ya juu.

Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu, Dk Nicas Yabu

Gavana Tutuba amewaonya wahitimu dhidi ya kushiriki vitendo visivyozingatia maadili kama wizi, udanganyifu na kusababisha mikopo chechefu, akibainisha kuwa BoT itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa wafanyakazi wa sekta ya fedha nchini na haitasita kuchukua hatua kali kwa wale watakaokiuka maadili ya kazi.

SOMA: BoT yaonya upotoshaji amana benki za biashara

Aidha, amewahimiza wahitimu kuwa wabunifu, wachapakazi na kutumia maarifa waliyoyapata kujiajiri au kutafuta fursa mpya katika soko la ushindani.

 

Amesema dunia ya sasa inahitaji watu wanaoweza kuwaza nje ya mifumo ya kawaida na kutumia ujuzi wa vitendo (competency-based learning) kuleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali.

Katika hotuba yake, Gavana Tutuba pia amesisitiza umuhimu wa wahitimu kuendelea kujiendeleza kitaaluma kwa kuwa mabadiliko ya teknolojia na maarifa yanakwenda kwa kasi.

Amesema kuhitimu sio mwisho wa safari bali ni hatua ya kwanza ya safari ndefu ya kujifunza.

Akizungumza awali, Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu, Dk Nicas Yabu, amesema kuwa Chuo hicho kinaendelea kuwa kitovu cha mafunzo ya kikanda ambapo katika mwaka 2024/25, jumla ya washiriki 127 walitoka nje ya nchi—ikiwemo Kenya, Uganda, South Sudan, Somalia, Burundi, Zambia, Zimbabwe, Comoros, Botswana na Ghana.

Uwepo wa washiriki hao wa kimataifa uliingizia Benki Kuu dola za marekani 93,500, hatua inayodhihirisha ukuaji na mvuto wa programu za mafunzo zinazotolewa na chuo hicho.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 36 wametunukiwa Stashahada ya Uendeshaji na Usimamizi wa Benki, huku wahitimu 31 wakitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Uongozi wa Benki.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. i get paid more than $90 to $120 per hour for working online. i heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    .this is what i do…. http://Www.Work84.Com

    1. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button