Geita, TMA hazijachana nyavu zao

TIMU za Geita Gold na TMA STARS zinazoshiriki ligi ya Championship ndizo pekee hazijaguswa nyavu zao kwenye Ligi hiyo katika michezo sita zilizocheza mpaka sasa.
Geita ambayo ni kinara wa ligi ikiwa na pointi 14 katika michezo sita, imeshinda minne na sare mbili, wakiwa hawajapoteza mchezo huku TMA ikishinda mitatu na sare tatu nayo pia haijapoteza mchezo ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 12 nyuma ya Mtibwa katika nafasi ya pili kwa pointi 13, ambayo imepoteza mchezo mmoja.
Kazi ipo katika mechi zijazo je, zutaweza kuendelea kulinda nafasi zao? Zikiteleza kidogo zinaweza kupishana nafasi nazo kutokana na utofauti mdogo wa pointi.
SOMA: Geita Gold yaitaka Ligi Kuu Tanzania Bara
Geita katika mchezo ujao Novemba 3 itakuwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kumenyana na Mbeya Kwanza katika mchezo ambao huenda ukawa mgumu kutokana na ubora wa kila moja.
Mtibwa Sugar itakuwa kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro Novemba 2 kuikaribisha Songea United inayofundishwa na kipa wa zamani wa Simba na Yanga Ivo Mapunda huku TMA ikitarajiwa kucheza na Mbuni mkoani Arusha Novemba 3.
Matokeo ya mechi hizo yanaweza kubadilisha msimamo au ukabaki kama ulivyo.
One Comment