KIKAO cha Kamisheni ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Geita kimeridhia majimbo mawili ya uchaguzi ya Chato na Busanda yagawanywe kupata majimbo manne ili kuchagiza maendeleo.
Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Mkoa wa Geita, Deodatus Kayango amewasilisha mapendekezo ya mkoa na kisha kuridhiwa na wajumbe wa kikao cha RCC kilichoketi maalum kwa ajili ya kujadili ajenda hiyo.
Kayango amesema mkoa huo umependekeza jimbo la Busanda ligawanywe kupata jimbo la Busanda na Jimbo la Butundwe (Katoro) huku jimbo la Chato likigawanywa kupata jimbo la Chato Kusini na Chato Kaskazini.
Amesema mapendekezo hayo yatakayotumwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) yamezingatia vigezo vinavyohitajika pamoja na taarifa rasmi kutoka kwenye vikao vya halmashauri husika.
K wa mujibu wa Kayango, Wilaya za Mbogwe na Bukombe hakukuwa na mapendekezo ya majimbo mapya huku wilaya ya Nyang’hwale ilikuwa na mapendekezo ya jimbo jipya la Kharumwa na Nyang’hwale yenyewe.
“Katika kigezo cha idadi ya watu, mjini wanatakiwa watu laki sita na vijijini watu laki nne, kwa jimbo la Busanda ilionekana kuna watu 671,761 na ni kijijini hivo tumeona limekidhi vigezo vya kugawanywa.
“Chato kuna idadi ya watu wapatao 584,963 kwa hiyo na wenyewe wamekidhi vigezo kwenye kigezo hicho tunaweza kupata jimbo la Chato Kaskazini na Chato Kusini. Jimbo la Nyanghwale kuna takribani watu 225,000 na kwa kigezo hicho inaonekana kabisa wazi kwamba haijakidhi vigezo vilivyowasilishwa,”amesema Kayango.
Kayango ameongeza kuwa kwa kigezo cha kiuchumi majimbo ya Chato na Busanda pia yamekidhi vigezo kwani yana vyanzo vingi vya mapato kutokana na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.
Katibu Tawala huyo msaidizi amesema kwa kigezo cha ukubwa wa eneo jimbo la Busanda litakuwa na kata 11, jimbo la Butundwe (Katoro) litakuwa na kata 11, Chato kasikazini itakuwa na kata 14 na Chato kusini kata tisa.
Amefafanua kuwa kwa kigezo cha kiutawala majimbo yote yatakayotenganishwa hayataingiliana na halmashauri ama majimbo mengine kwa hivo itarahisisha utawala wa viongozi na uwakilishi kwa wananchi.
Mwanasheria wa Mkoa wa Geita, Sarah Mwangole amesema mapendekezo yote yamezingatia sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024, chini ya kanuni ya Tume Huru ya Uchaguzi ya 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amezitaka halmashauri husika ambazo zimependekeza majimbo mapya kuendelea kuwa na utulivu ili kusubiri matokeo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!
Visit This…… http://www.worksprofit7.com/