Gugu: Umoja ni ufanisi katika majukumu

DODOMA: Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuendelea kudumisha mshikamano, upendo na ushirikiano kazini, akisisitiza kuwa umoja wao ndio msingi wa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

Gugu amesema wakati akifungua rasmi Kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Msalato, jijini Dodoma, leo Januari 10, 2026.

Akizungumza katika kikao hicho, Gugu amesema Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu linalowawezesha watumishi kushiriki kikamilifu masuala muhimu ya utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ameeleza kuwa kikao hicho ni cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kimeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa mpango wa bajeti wa wizara katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, 2025 pamoja na kujadili mikakati ya utekelezaji kwa kipindi kinachofuata.

Kadhalika, Gugu amesisitiza umuhimu wa viongozi na wafanyakazi kuendelea kushirikiana na kusaidiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, akieleza kuwa kudumisha utu, maadili mema na utendaji kazi wenye staha utaisaidia wizara ya hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na tija zaidi.




l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com