Guterres apinga udhibiti wa Gaza

NEW YORK : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ametoa wito kwa Israel kuachana na mpango wake wa kuuteka na kuudhibiti Mji wa Gaza, huku kukiwa na hofu ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Akizungumza na waandishi habari, Guterres amesema maelfu ya raia wa Gaza watalazimika kukimbia tena, na kuzitumbukiza familia katika hatari kubwa zaidi. Hatahivyo, Guterres ameendelea kutoa  wito wa kusitisha mapigano mara moja na kuwaomba wadau kuendelea kutoa misaada ya kibinadamu.

Jumatano ya wiki hii ,Msemaji wa jeshi la Israel alitangaza kuwa maandalizi yanaendelea kwa ajili ya mpango wa kuwahamisha wakaazi wa Gaza. SOMA: Guterres aitisha msaada wa kimataifa

Waziri wa Fedha wa Israel, Bezalel Smotrich ameitaka serikali ya nchi hiyo kuanza kujinyakulia sehemu ya maeneo ya Ukanda wa Gaza, iwapo kundi la wanamgambo la Kipalestina la Hamas, litaendelea kukataa kuweka chini silaha.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button