Guterres akataa pednekezo la Trump

NEW YORK : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelikataa pendekezo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kudhibiti Gaza na kuwahamisha Wapalestina.

Katika mkutano na waandishi wa habari alikokuwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, Trump alipendekeza Marekani kuwa na umiliki wa muda mrefu wa Gaza, jambo lililokosolewa vikali na jumuiya ya kimataifa.

Guterres alisema katika kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za Wapalestina kwamba haki za Wapalestina zinahusisha kuishi kwa uhuru katika nchi yao, lakini haki hizo zimekuwa zikididimiza.

Advertisement

Pia  amesema  suluhisho la kudumu linahitajika kupatikana kwa mataifa mawili, ambapo Israel na Palestina wangeishi kwa amani. Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alisema hatua yoyote ya kuwahamisha Wapalestina ni “safisha safisha ya kikabila”, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za kimataifa.

Baada ya ukosoaji mkubwa, maafisa wa Trump walijitetea, wakisema kuhamisha Wapalestina kutakuwa kwa muda tu, na hakutakuwa na kupeleka wanajeshi kutekeleza mpango huo.

SOMA: UN kujadili mizozo duniani

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *