Haaland moto otea mbali

ERLING Haaland aliendelea na mwanzo mzuri msimu huu kwa kupiga hat-trick mfululizo huku mabingwa watetezi Manchester City wakiwachapa West Ham United mabao 3-1 uwanja wa London.

Mshambuliaji huyo wa Norway alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuongeza la tatu dakika ya 83 na hivyo kufikisha mabao saba katika mechi tatu na kudumisha mwanzo wa City kwa 100% kwenye kampeni za mbio za ubingwa.

SOMA: Haaland nje hadi Februari

Haaland alianza kufunga dakika ya 10 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bernardo Silva, lakini West Ham walisawazisha baada ya Ruben Dias kujifunga kutokana na krosi ya Jarrod Bowen.

Haaland aliongeza bao la pili dakika ya 30.

SOMA: Haaland huyu ni tatizo EPL

Ushindi huo unamaanisha kuwa kikosi cha Pep Guardiola tayari kiko kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu  wakiwa na pointi tisa, huku West Ham wakiwa katika nafasi ya 14 wakiwa na pointi tatu katika mechi tatu walizocheza.

Habari Zifananazo

Back to top button