Halmashauri zaagizwa kuzingatia maagizo ya CAG

ARUSHA: KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa ameiagiza Halmashauri ya Meru na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC kuhakikisha wanasimamia maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) ili kupunguza hoja ikiwemo kutumia vema fedha za bakaa katika miradi ya maendeleo

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Katibu Tawala, Musa wakati wa ukaguzi wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023/24 katika halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha DC.

 

Amesema Halmashauri ya Meru bado inahoja ya Sh milioni 514 inadaiwa ambazo ni fedha za mikopo ya 10% waliyoitoa kwa ajili ya mikopo ya mikopo na kumwagiza Mkurugenzi wa Halmahera hiyo, Zainabu Makwinya kuhakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ili fedha wanazotoa kwa ajili ya mikopo ya asilimia kumi zirejeshwe kwa wakati

Naye, Mkaguzi wa Nje Mkoa wa Arusha, Valence Rutakyamirwa ameshauri ukarabati wa madarasa ufanyike ikiwemo miradi midogo midogo ya Sh milioni 2 hadi nane itekelezwe ili isije kuharibika na badae halmashauri hiyo kuingia hasara kubwa zaidi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Makwinya amesema ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo ni mzuri hadi kufikia Sh bilioni 7.6 na kusisitiza kushirikiana zaidi katika utendaji.

SOMA ZAIDI

RAS Arusha ataka mikopo ikusanywe iwafaidishe wengine

Wakati huo huo akiwa Haalmashauri ya Arusha DC, Mkaguzi wa Nje, Valence Rutakyamirwa aliishauri halmashauri hiyo kuchanganua madeni ya zamani na kuyaingiza katika mfumo wa TAUSI na yasiyokuwa halali yafutwe.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC Suleiman Msumi amesema halmashauri hiyo itaendelea kujitahidi kuhakikisha hoja za ukaguzikuletwa zinapungua ikiwemo kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button