Jiografia (CBG). Baadaye alihamia Shule ya Sekondari Milambo, mjini Tabora na kuhitimu kidato cha sita kwa daraja la pili.
Alivyokosa ada
Safari yake kitaaluma iliendelea hadi mwaka 2006 alipojunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusoma Shahada ya Science in Aquatic Environmental Science. Hata hivyo kabla ya muhula wa kwanza kuisha, yeye na baadhi ya wanafunzi walisimamishwa masomo kwa sababu za kutolipa ada.
“Kama utakumbuka vizuri mwaka huo mambo ya mikopo ya Elimu ya juu yalisumbua sana na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia wa wakati huo Profesa Peter Msolla alitangaza kwamba wavulana wenye ufaulu wa daraja la pili wasingepewa mikopo,” anasema.
Anasema, “Jambo hilo liliniumiza sana katika maisha yangu. Tulitakiwa kurudi nyumbani kwa ahadi kwamba mwaka unaofuata tutapewa mikopo na kuendelea na shule. Tulitakiwa kuahirisha masomo.”
Mwaka 2007 alirudi chuoni kuendelea na masomo. Ingawa alipenda kuendelea na shahada aliyokuwa akisoma, alishauriana na wanafunzi wenzake wakaona ili kuhakikisha mwaka unaofuata wanaendelea na chuo, waombe pia shahada ambazo upo uhakika wa kupata mkopo.
Aliamua kuomba Shahada ya Sayansi ya Ualimu. “Niliumia sana, niliambiwa kama nataka kusoma ile shahada basi niahirishe tena mwaka mwingine hadi mwaka unaofuata na sikuwa tayari basi nikalazimika kuendelea na shahada ya sayansi na elimu.”
Alihitimu chuoni hapo mwaka 2010 kwa ufaulu wa daraja ya pili la juu. Aliingia mtaani na kufanya kazi kadhaa kabla ya kupata udhamini wa Serikali ya China kwenda kusoma Shahada ya Pili mwaka 2011. Lakini kutokana na sababu mbalimbali, hakwenda mwaka huo.
Mwaka uliofuata, aliomba udhamini sehemu mbalimbali, akafanikiwa kupata sehemu tatu tofauti; mbili zikiwa nje ya nchi na moja ya nchini.
Baada ya kujadiliana na familia, aliamua kwenda China katika chuo cha Northeast Normal kilichopo mjini Changchun Jimbo la Jilin ambako alisoma Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika ikolojia.
“Nilimaliza digrii yangu na kufanya vizuri sana kiasi ambacho kilimfanya mwalimu wangu kuandika barua rasmi kwa chombo kinachohusika na kutoa udhamini wa serikali ya China yaani Chinese Government Scholarship Council wa kuendelea na shahada yangu ya Uzamivu (PhD).”
kuonekana kwa mnyama huyo mahali hapo na kufanikiwa kuchapisha utafiti huo katika jarida la kimataifa la Zuolojia la Pakistani.
Chapisho lilionesha uwapo wa mbwa mwitu katika eneo la milima ya Khingan, katika hifadhi ya Hanma iliyopo mji mdogo wa Jinhe jimboni Inner Mongolia.
Katika utafiti huu pia nilishirikiana na watafiti wenzangu wa kichina. Ila napenda kumtambua kwa karibu mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Pensylvania State cha Marekani, Dk Asia Murphy kwa ushirikiano wake mkubwa wakati tukiandika kazi hii.
Taarifa za ushindi nilizipokea kupitia kwa rafiki yangu Mchina anayeishi jimbo la Inner Mongolia. Nilitumiwa tangazo na rafiki zangu wa kichina wakinieleza juu ya suala hilo. Nilijua nina vigezo vyote na tangu siku ya kwanza nilihisi ningeweza kushinda.
Tunashukuru Mungu tumeshinda. Walioratibu shindano ni taasisi ya hifadhi za asili jimboni humo na hivyo tuzo ilitolewa na viongozi kutoka taasisi hiyo. Kwa sasa nasubiri kuipokea ana kwa ana kwa sababu hivi sasa nipo Tanzania.
Pamoja na chapisho hilo lililonipa ushindi, nimechapisha zaidi ya machapisho manane na yote nikiwa kama mchapishaji wa kwanza na yote yanahusu tabia, uhusiano, uwapo, mazingira na maisha ya wanyamapori kwa jumla.
Siri ya mafanikio
Tuzo niliyoshinda ilikuwa ikishindaniwa na watafiti kutoka mataifa mbalimbali duniani. Wala sikuwa na woga wowote. Imani yangu siku zote huwa ni kwamba kama unajiamini unaweza jambo fulani, ingia.
Siku zote hakuna kushindwa bali kuna kushinda au kujifunza.Siyo kwamba kila nikishiriki nashinda. La hasha! Nimeshiriki pia tuzo mbalimbali na kukosa. Huwa nikikosa, kuna kitu najifunza na kinanisaidia mbele ya safari.
Mfano, mwaka juzi tulishiriki na mtafiti mwenzangu wa Marekani kwa pamoja kwenye kuomba fedha inayotolewa na shirika maarufu la mambo ya wanyamapori duniani na hatukubahatika kushinda lakini tulijifunza mengi sana.
Mwaka jana tulishiriki kupitia shindano lingine tukashinda japo haikuwa na ufadhili mzuri. Kilichonifanya kujiamini zaidi mara hii nadhani ni namna watu wa China walivyopokea taarifa za uwapo wa mnyama huyo eneo hilo. Ziliwafurahisha sana na taarifa kurushwa na televisheni ya CCTV ya nchini humo. Ilinipa imani sana.
Siri kubwa ya mafanikio ni kupenda unachofanya na kumtanguliza Mungu. Siyo kwamba mimi ni bora zaidi kuliko wale wenzangu. Kuna mambo mengi unatakiwa kufanya ili utafiti wako uweze kuwa na matunda mazuri ikiwamo jinsi unavyopangilia utafiti wako vizuri
Lazima usome maandiko mbalimbali na kwa uzuri ujue ni eneo gani, saa ngapi, muda gani wa mwaka ukiweka kamera zako unaweza kupata picha/video za wanyama fulani kama wapo.
Hapo hasa ndipo unapotakiwa kuchanga karata zako vizuri na nafikiri hapo ndipo nilipokuwa tofauti na wengine na hatimaye kufanikiwa kumnasa mnyama huyo ambaye hakukuwa na ushahidi usiona shaka wa uwapo wake tangu mwaka 1972 kwa mujibu wa maandiko ya wenyeji wa maeneo hayo.
Utafiti wangu una maana kubwa kwa ikolojia ya wanyama mahali hapo ukizingatia wolf ni mmoja wa wanyama wa juu kabisa kwa walao wenzao eneo hilo. Hivyo ana mdhara makubwa kwa mfumo mzima wa maisha mahali hapo.
Kubwa zaidi, kiutalii, utafiti huu ni jambo kubwa sana. Utasaidia sana kutengeneza fedha kwa watalii wengi kwenda kwa lengo la kuona wolf siku zijazo na hivyo kukuza uchumi wa jimbo kwa jumla.
Nikakumbuka nilikuwa mwindaji mzuri utotoni na nilipenda sana wanyama. Nikamwandikia kisha akasema basi nafikiri ukisoma chochote kinachohusu masuala haya utafanya vizuri.
Bila kuwasahau ndugu zangu wote na familia yangu, akiwamo mdogo wangu Columbas, kwa ujumla kila mara wamekuwa wakinitia nguvu.
Anachopenda, asichopenda
Katika mahojiano na Hamenya ambaye sasa anaishi Arusha akisubiri kurudi China kumalizia masomo yake ya PhD, nabaini mambo anayopenda na asiyopenda.
Zamani alipendelea muziki. Ndiyo maana aliibuka kuwa mchezaji wa ngoma mzuri wakati akiwa sekondari hata akapewa tuzo katika Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari (Umisseta).
Lakini sasa anapendelea kuangalia mpira wa miguu akisema hicho ndicho kilevi chake kikubwa. “Kwa maana sinywi pombe…Sijawahi kunywa pombe. Mpira naupenda sana na ndicho kitu kinachoniburudisha zaidi.” Anataja timu anazoshabikia kwa Tanzania ni Yanga. Timu za nje ni Liverpool ya Uingereza ambayo ikifungwa, huhisi kuugua.
Kitu kingine anachopenda ni siasa. Anasema siasa ni mfumo wa maisha ya watu. “Wengine huniambia kwamba mimi ni mtaalamu mzuri hivyo niachane na mambo ya siasa nisaidie taifa. Jibu langu huwa ni hili, ukiona msomi anaingia kwenye siasa na anashindwa kusaidia taifa basi hiyo ni shida yake binafsi na siyo shida ya wasomi wote.”
“Mimi binafsi nina malengo makubwa na taifa hili, siku nikipata nafasi yoyote ya uongozi serikalini nina hakika nitaonesha mfano mzuri sana,” anasema Hamenya akisisitiza kuwa ana ndoto kubwa kwa taifa taifa lake na kwamba ndiyo maana anafanya kila awezalo kuitangaza Tanzania kimataifa.
Hamenya anapenda pia kujenga urafiki na watu wengi zaidi duniani jambo analosema kuwa amefanikiwa kwani ana marafiki wa karibu anaoshirikiana nao mambo mbalimbali hasa kwenye sayansi na utafiti takribani katika mabara yote duniani.
Kuhusu mambo asiyopenda, Hamenya anasema “Kwa ujumla sipendi watu wavivu na wasiopenda maendeleo ya wenzao… Lakini pia sipendi watu na hasa viongozi wasiotimiza ahadi zao.”